Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino aliyekuwa ametiwa mbaroni kwa mara ya pili Jumatano tarehe 27 Septemba ameanzia mashtaka mapya Alhamisi tarehe 28 asubuhi. Mheshimiwa Owino alitiwa mbaroni Jumatatu tarehe 25 kwa matamshi yake ya cheche za matusi kwa rais Uhuru Kenyatta na familia yake amezuiliwa katika seli ya mahakama ya Kibera jijini Nairobi. Waendeshaji wa mashtaka walieleza korti kuwa wananuia kumshtaki mheshimiwa Owino kwa kumshambulia na kumuumiza mpiga kura bwana Joshua Otiende. Kulingana na maafisa waliopekua kesi hii wanasema kuwa Joshua Otiende alizuiwa na mheshimiwa Babu Owino kupiga kura yake hivi basi kumnyima uhuru wa kupiga kura. Makosa aliyodaiwa kutenda mheshimiwa Babu Owino aliyatenda katika ukumbi wa kijamii wa Soweto uliokuwa stesheni ya wapiga kura mnamo Agosti 8 siku ya uchaguzi mkuu. Ni wakati wa kikao cha Alhamisi tarehe 28 asubuhi, mwendeshaji wa mashtaka aliuliza korti kuhairisha ombi la mheshimiwa Babu Owino mpaka saa tano asubuhi. Mwendeshaji huyo wa mashtaka alisema kuwa mwandamizi wake ndiye atakuja kuongoza mashtaka ya kesi hiyo. Hali kadhalika wanasheria James Orengo, Otiende Amollo na Nelson Havi wanamwakilisha mheshimiwa Babu Owino kortini. Maafisa wa polisi waliimarisha usalama pale kortini na mazingira yake baada ya wanaomuunga mkono Babu Owino kujumuika na kuungana kupinga kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka kwake. Kwa sauti za juu walisema kuwa wanamtaka mheshimiwa Babu Owino wala hawaogopi vitoa machozi. Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nairobi aliwarai maaskari wa kupambana na ghasia wasiwarushie wanaoandamana vitoa machozi.

Na Wangu Kanuri.

 

LEAVE A REPLY