Na Wangu Kanuri. Ni aibu ghaya mwajiriwa yeyote kuripoti kazini akiwa mlevi. Licha ya kuonyesha udororaji wa tabia, utendakazi wa mwajiriwa mhusika hudidimia. Katika Kaunti ya Nakuru eneo bunge la Gilgil mkuu wa tume ya kuwaajiri walimu bi Nancy Macharia amekumbana na ulevi wa mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Mawaka  Jumatatu tarehe 13. Mwalimu huyu aliyekuwa amelewa chakari hakusita kujitetea akisema kuwa hajalewa bali aliamka akiwa amechelewa na kuharakisha kuchukua karatasi za mtihani wa kitaifa. Isitoshe mwalimu huyu alivurugana kimatamshi na mkurugenzi mkuu wa tume hiyo ya TSC bwana Christopher Maisiba ambaye hakughadhabishwa na mwalimu Masiba. Juhudi za mwalimu Masiba kuonyesha kuwa hakubugia pombe yoyote ile hazikufua dafu na akakamatwa kupitia amri za kamishina wa kaunti ya Nakuru bwana Joshua Nkanatha.

 

LEAVE A REPLY